Hadithi za Ufanisi

Toting Craft Hanno (Mfungwa)

Utekaji na Mauaji ya Wamarekani Filipino

TKM ililipa tuzo ya dola laki moja kwa habari zilizopelekea kukamatwa kwa gaidi wa kundi la Abu Sayyaf (ASG) Toting Hanno nchini Filipino.

Toting Craft Hanno alikuwa mwanachama wa ASG aliyeshiriki kwenye utekaji nyara wa raia watatu wa Marekani kutoka eneo la mapumziko ya kitalii la Dos Palmas nchini Filipino mnamo tarehe 27 mwezi Mei, mwaka 2001. Wamerikani hao watatu walitajwa kama Guillermo Sobero na Martin na Gracia Burnham, mume na mke wamishenari. Mnamo tarehe 11 mwezi Juni mwaka 2001, msemaji wa kundi la ASG Abu Sabaya alitangaza kwamba Guillermo Sobero alikuwa ameuliwa kama “zawadi ya siku ya kuzaliwa” kwa Rais wa Filipino Gloria Macapagal-Arroyo. Tarehe 7 Oktoba 2001, fuvu la binadamu lilipatikana kwenye kisiwa cha Basilan ambalo lilithibitishwa kuwa lile la Guillermo Sobero. Mwezi Juni 2002, Martin Burnham alifariki kwenye mashambulio ya risasi kati ya askari wa Filipino na kundi la ASG; Gracia Burnham alijeruhiwa lakini aliokolewa na kurejeshwa Marekani.

Mnamo tarehe 6 Januari mwaka 2005, vikosi vya usalama vya Filipino, kufuatilia taarifa ya kijumbe mtoa habari, vilimkamata Hanno.

Skip to content