Hadithi za Ufanisi

Khadaffy Janjalani (Marehemu)

Utekaji na Mauaji ya Wamerikani Filipino

TKM ililipa tuzo ya dola milioni tano kwa watu wawili waliotoa habari juu ya kiongozi wa kundi la Abu Sayyaf Group (ASG) Khadaffy Janjalani. Mnamo tarehe 7 mwezi Juni mwaka 2007, Balozi wa Marekani nchini Filipino aliongoza shughuli ya kuwasilisha tuzo kwa watu hao kwenye sherehe ya hadhara katika kisiwa cha Jolo.

Khadaffy Janjalani alikuwa mmoja wa vinara wa juu zaidi wa kundi la kigaidi la ASG lenye makao yake nchini Filipino. Janjalani alihusika kwenye utekaji na mauaji ya raia wa Filipino na Marekani. Alihusishwa na utekaji wa Martin na Gracia Burnham na raia wengine wawili Wamarekani, na alihusika moja kwa moja na ukataji kichwa wa raia wa Marekani Guillermo Sobero. Janjalani pia alipanga na kutekeleza mashambulio mengi dhidi ya maslahi ya Marekani, pamoja na njama dhidi ya Ubalozi wa Marekani mjini Manila, uzamishaji mwaka 2004 wa Superferry 14, na ulipuaji wa bomu mara tatu siku ya Valentine mwaka 2005 ambao kwa jumla uliua au kujeruhi mamia ya watu wasiokuwa na hatia.

Mnamo tarehe 4 mwezi Septemba mwaka 2006, majeshi ya Filipino yakifuatilia habari zilizotolewa na watu kadhaa yalizindua operesheni kumkamata Janjalani. Wakati wa operesheni, iliripotiwa kwamba Janjalani alijeruhiwa vibaya lakini akatoroka. Katika miezi iliyofuata, uvumi uliibuka kuhusu kifo cha Janjalani. Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2007, watu wawili walijitokeza na habari kuhusu ulipokuwapo mwili wa Janjalani. Baada ya upimaji wa DNA, shirika la FBI lilithibitisha kwamba Janjani alikuwa amekwisha kufa kwa kweli. Habari zote zilizotolewa na watu hawa zilithibitika kuwa muhimu kuhusu mahali alikokuwa na hatimaye kutambuliwa kwake Janjalani.

Skip to content