Utekaji nyara na Mauaji ya Wamarekani nchini Filipino

TKM ililipa tuzo ya dola milioni moja kwa ajili ya habari zilizopelekea kupatikana kwa kamanda wa kundi la Abu Sayyaf (ASG) Hamsiraji Sali.
Hamsiraji Sali alishiriki kwenye utekaji nyara wa Jeffrey Schilling na kundi la ASG tarehe 28 Agosti mwaka 2000, na tukio la utekaji nyara Dos Palmas mnamo tarehe 27 Mei, 2001. Badala ya Jeffrey Schilling, ASG ilidai dola milioni kumi na kuachiwa huru magaidi wa kimataifa watatu kutoka magereza ya Marekani: wanamgambo wa al-Qa’ida Ramzi Yousef, Wali Khan, na Omar Abd al-Rahman (kwa jina jingine “Shehe Kipofu”) kiongozi wa kiroho wa kundi la kigaidi la Misri al-Gama’at al-Islamiyya.
Mnamo tarehe 12 Aprili 2001, Jeffrey Schilling alifaulu kuwakwepa watekaji wake wakati wa uvamizi wa majeshi ya Filipino kwenye kambi ya ASG alipokuwa ameshikiliwa na kurejeshwa Marekani.
Mnamo tarehe 27 Mei, 2001, kundi la ASG liliwateka nyara raia watatu wa Marekani kutoka eneo la Mapumziko ya kitalii la Dos Palmas, Palawan, nchini Filipino. Wamarekani watatu hao walitajwa kama Guillermo Sobero na Martin na Gracia Burnham, mume na mke wamisionari. Tarehe 11 Juni, 2001, msemaji wa kundi la ASG Abu Sabaya alitangaza kwamba Guillermo Sobero alikuwa ameuliwa kama “zawadi ya siku ya kuzaliwa” kwa Rais wa Filipino Gloria Macapagal-Arroyo. Tarehe 7 Oktoba 2001, fuvu la binadamu lilipatikana kwenye kisiwa cha Basilan ambalo lilithibitishwa kuwa lile la Guillermo Sobero. Mwezi Juni 2002, Martin Burnham alifariki kwenye mashambulio ya risasi kati ya askari wa Filipino na kundi la ASG; Gracia Burnham alijeruhiwa lakini aliokolewa na kurejeshwa Marekani.
Mnamo mwezi Februari 2002, Sali alishitakiwa rasmi na baraza la uchunguzi wa awali la Shirikisho la Marekani mjini DC kwa makosa yafuatayo: Njama Isababishayo Mauti; Kuchukua Mateka na makosa matatu ya Kuchukua Mateka Kusababishako Mauti. Mnamo tarehe 8 Aprili 2004, makomando skauti wa jeshi la nchi kavu la Filipino, kufuatilia habari zilizotolewa na watoaji habari wengi, walizindua operesheni ya kumkamata Sali, ambaye aliuliwa kwenye mapigano ya risasi na wanajeshi hao.
Wasilisha Kidokezi
Fanya jukumu lako. Dhamini ulimwengu salama na siku angavu zijazo. Bonyeza kujifunza kuhusu chaguzi za kuripoti vidokezi vya Tuzo kwa Mahakama.
- watekwa nyara/Utekaji nyara
- Korea Kaskazini
- Kuingilia Uchaguzi
