Hadithi za Ufanisi

Edgar Gustavo Navarro (Marehemu)

Utekeji Nyara wa Wamarekani Kolombia

TKM ililipa tuzo ya jumla ya dola laki tisa kwa watu watatu waliotoa taarifa kuhusu alipokuwa Edgar Navarro, kamanda wa Majeshi ya Mapinduzi ya Kolombia (FARC).

Mnamo mwezi Februari 2003, Thomas Howes, Keith Stansell, na Marc Gonsalves walitekwa nyara na FARC ndege yao ilipoanguka katika msitu wa Kolombia. FARC na wala njama wenzake waliwaua abiria wengine wawili wa ndege hiyo, raia wa Marekani Thomas Janis na mwananchi wa Kolombia Sajini Luis Alcides Cruz.

Navarro, naibu kamanda wa kikosi cha FARC cha Teofilo Forero Mobile Column, alituhumiwa kushiriki kwenye utekaji nyara huo.

Mnamo tarehe 19 mwezi Oktoba, 2003, watoa taarifa watatu, wakihamasishwa na uwezekano wa kupata tuzo, waliongoza timu ya wanajeshi wa Kolombia kwenda kambi ya Navarro kwa jaribio la kumkamata yeye na wanachama wengine wa FARC. Navarro aliuliwa kwenye mapigano ya risasi na askari wa jeshi la nchi kavu. Wamarekani hao watatu waliokolewa baada ya hapo mnamo tarehe 2 mwezi Julai 2008 kwenye operesheni ya wanajeshi wa Kolombia.

Skip to content