Utekaji Nyara na Mauaji ya Wamarekani Filipino

TKM ililipa tuzo ya dola milioni tano kwa watu wawili waliotoa habari juu ya kiongozi wa kundi la Abu Sayyaf (ASG), Abu Solaiman. Mnamo tarehe 7 mwezi Juni, mwaka 2007, Balozi wa Marekani nchini Filipino aliongoza shughuli ya kuwasilisha tuzo kwa watu hao kwenye sherehe ya hadhara katika kisiwa cha Jolo.
Abu Solaiman alikuwa mmoja wa vinara wa juu zaidi wa ASG, kundi la kigaidi linaloendesha shughuli zake Filipino. Solaiman, pamoja na Khadaffy Janjalani, alihusika na utekaji nyara na mauaji ya raia wa Filipino na Marekani. Solaiman alihusishwa kwenye utekaji wa Martin na Gracia Bumham na raia wengine wawili wa Marekani na alishiriki kwenye ukataji kichwa wa raia wa Marekani Guillermo Sobero. Solaiman pia alikuwa amepanga na kutekeleza mashambulio dhidi ya maslahi ya Marekani, kama vile njama za kulipua bomu dhidi ya Ubalozi wa Marekani mjini Manila, uzamishaji mwaka 2004 wa Superferry 14, na ulipuaji wa bomu mara tatu siku ya Valentine mwaka 2005 ambao kwa jumla uliua au kujeruhi mamia ya watu wasiokuwa na hatia.
Mnamo tarehe 16 Januari mwaka 2007, majeshi ya Filipino, yakifuatilia habari zilizotolewa na watoa habari, yalizindua operesheni kumkamata Solaiman. Wakati wa uvamizi, Solaiman alipinga kukamatwa kwake na aliuliwa.
Wasilisha Kidokezi
Fanya jukumu lako. Dhamini ulimwengu salama na siku angavu zijazo. Bonyeza kujifunza kuhusu chaguzi za kuripoti vidokezi vya Tuzo kwa Mahakama.
- watekwa nyara/Utekaji nyara
- Korea Kaskazini
- Kuingilia Uchaguzi
