Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Yasin Kilwe, kiongozi wa mkoa wa kundi la al-Shabaab lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni (FTO). Akijulikana pia kama Yasin Usman Kilwe na Yasin Khalid Osman, Kilwe ndiye shekhe wa al-Shabaab eneo la Puntland kaskazini mwa Somalia na ametuhumiwa kwa kupanga mashambulio yaliyowalenga maofisa wa Puntland.
Kabla ya kujiunga na al-Shabaab, Kilwe alikuwa kiongozi wa wanamgambo wa ndani eneo la Vilima vya Galgala kaskazini mwa Somalia. Kundi hilo la wanamgambo liliripotiwa kutwaa ardhi kwenye eneo la Vilima na kutekeleza shambulio baya dhidi ya kambi ya kijeshi kwenye eneo hilo.
Mnamo mwaka 2012, wanamgambo wa Kilwe walijiunga rasmi na al-Shabaab, ambayo iliahidi utii kwa al-Qa’ida (AQ) mwezi huo huo. Kuungana huko kuliipa al-Shabaab, na kwa namna fulani AQ, kikosi cha kivita chenye nguvu.
