Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu Matukio ya Mabomu ya Barua. Kati ya mwezi Disemba, mwaka 1996 na mwezi Januari, mwaka 1997, mabomu 16 ya barua yaliyofichwa kuonekana kama kadi za sikukuu yalipelekwa kupitia huduma ya barua kwa wapokeaji nchini Marekani na Uingereza.
Kati ya mabomu hayo ya barua, 13 yalipokelewa kwenye ofisi za gazeti la al-Hayat katika miji ya New York, mjini Washington, D.C., na mjini London. Bomu moja lililipuka mjini London, likawajeruhi vibaya watu wawili. Mabomu yale mengine matatu yaligunduliwa kwenye gereza la serikali kuu ya Marekani mjini Leavenworth, Kansas.
Kila moja la mabomu hayo ya barua lilikuwa na mhuri wa posta ya Alexandria, Misri, wa mnamo tarehe 21 mwezi Disemba, mwaka 1996, na hakuna hata moja lililokuwa na anwani ya kurejesha. Mabomu hayo yalikuwa ndani ya bahasha za kawaida nyeupe na anwani zilizotokana na kompyuta na alama nyingine anuwai.
