Utekaji Nyara wa ndege ya Pan Am Flight 73

Asia Kusini na Kati | Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo ka Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu utekaji nyara wa Ndege ya Pan Am 73. Mnamo tarehe 5 mwezi Septemba, mwaka 1986, watu walioshukiwa kuwa wanachama wa Shirika la kigaidi la Abu Nidal waliteka nyara Ndege ya Pan Am 73 ikiwa ardhini mjini Karachi, Pakistani, ikiwa na watu 379. Baada ya kuwashika mateka abiria na wahudumu kwa karibu saa 16, watekaji nyara hao walianza kufyatua risasi kiholela. Watu ishirini, wakiwamo Wamarekani wawili, waliuliwa na wengine zaidi ya 100 wakajeruhiwa.

Magaidi watano walioshiriki katika utekaji nyara huo hatimaye walinaswa, wakashtakiwa, na wakahukumiwa kufungwa gerezani nchini Pakistani. Hata hivyo, wanne kati ya waliopatikana na hatia waliripotiwa kuachiliwa huru kutoka kizuizini mnamo mwezi Januari, mwaka 2008 na wangali huru. Kila mmoja alifunguliwa rasmi mashtaka na jopo kuu la mahakama ya serikali kuu ya Marekani na yupo kwenye Orodha ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi ya Shirika la FBI. Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo za hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu kila mmoja wa watu hawa:

  • Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki
  • Jamal Saeed Abdul Rahim
  • Muhammad Abdullah Khalil Hussain ar-Rahayyal
  • Muhammad Ahmed al-Munawar

Skip to content