Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu utekaji nyara na mauaji ya mwaka 2003 ya raia wa Marekani nchini Kolombia. Mnamo tarehe 13 mwezi Februari, mwaka 2003, ndege ya serikali ya Marekani iliyokuwa katika shughuli ya kukabiliana na dawa za kulevya ilitua kwa dharura mjini Caqueta, nchini Kolombia. Wanachama wa kundi la waasi la mrengo wa kushoto nchini Kolombia linalojulikana kama Vikosi vya Kimapinduzi vya Kolombia (FARC) walimuua raia wa Marekani Thomas Janis na Mkolombia Sajini Luis Alcides Cruz. Waasi hao waliwateka raia wengine watatu wa Marekani waliokuwa ndani ya ndege hiyo: Marc Gonsalves, Thomas Howes, na Keith Stansell.
