Utekaji Nyara na Mauaji ya Peter Kilburn

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu utekaji nyara na mauaji ya Peter Kilburn. Kilburn alikuwa mkutubi maktaba ya Chuo Kikuu cha Kimarekani cha Beirut. Mnamo tarehe 3 mwezi Disemba, mwaka 1984, aliripotiwa kutoweka. Miezi kumi na sita baadaye, mwili wake ulipatikana pamoja na miili ya mateka wengine wawili. Wahanga hao walikuwa wamepigwa risasi na kutupwa milimani mashariki mwa Beiruti. Kilburn alikuwa miongoni mwa wahanga 100, wengi wao kutoka mataifa ya Ulaya Magharibi, ambao walitekwa nyara na magaidi wa Hizballah na washirika wao na kuzuiliwa wakati wa mgogoro wa mateka Lebanoni uliodumu kwa muongo mmoja.

Skip to content