Utekaji Nyara na Mauaji ya Lebanon

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu utekaji nyara na mauaji ya Wamarekani nchini Lebanoni kutoka mwaka 1982 hadi mwaka 1992. Wakati wa kipindi hiki, Hizballah na magaidi waliohusishwa na Hizballah waliwateka nyara na kuwashikilia mateka karibu watu 100 wa mataifa ya kigeni, wengi wao kutoka mataifa ya Magharibi. Miongoni mwa waathiriwa wa utekaji nyara huo, Wamarekani William Buckley, Peter Kilburn, na William Higgins waliteswa na kuuliwa.

William Buckley alikuwa mkuu wa kituo cha CIA nchini Lebanoni, jukumu alilojitolea kuchukua baada ya shambulio la bomu la mwaka 1983 dhidi ya Ubalozi wa Marekani jijini Beiruti ambalo liliwaua watu 63, wakiwamo Wamarekani 17. Mnamo tarehe 16 mwezi Machi, mwaka 1984, Buckley alitekwa nyara mjini Beiruti akielekea kazini. Buckley alihojiwa na kuteswa kabla ya kufa akishikiliwa mateka mnamo tarehe 3, mwezi Juni, mwaka 1985.

Peter Kilburn alikuwa mkutubi Chuo Kikuu cha Kimarekani cha Beiruti. Mnamo tarehe 3 mwezi Disemba, mwaka 1984, aliripotiwa kutoweka. Miezi kumi na sita baadaye, mwili wake ulipatikana pamoja na ile ya mateka wengine wawili. Wahanga hao walikuwa wamepigwa risasi kisha wakatupwa milimani mashariki mwa Beirut.

Mwanajeshi wa Kikosi cha Marine Corps cha Jeshi la Marekani Kanali William Higgins alikuwa mmoja wa washiriki wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kusini mwa Lebanoni alipotekwa nyara mnamo tarehe 17 mwezi Februari, mwaka 1988. Watekaji wake walimtesa na kumhoji Higgins kabla ya kumuua.

Skip to content