Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu utekaji nyara na mauaji ya Daniel Pearl. Pearl, Mkuu wa Ofisi ya Asia Kusini ya gazeti la Wall Street Journal, alitekwa nyara mjini Karachi, Pakistani, mnamo tarehe 23 mwezi Januari, mwaka 2002. Mnamo mwezi Februari mwaka 2002, video ilichapishwa mtandaoni ikionyesha mauaji yake. Mabaki ya Pearl yalipatikana mnamo mwezi Mei, mwaka 2002 na yakarejeshwa Marekani.
Mnamo mwezi Juni, mwaka 2002, Ahmed Omar Saeed Sheikh alifunguliwa rasmi mashtaka nchini Marekani kwa utekaji-mateka na njama ya kufanya utekaji-mateka, matendo yaliyosababisha mauaji ya Pearl, na vilevile utekaji nyara wa mwaka 1994 wa raia mwingine wa Marekani nchini India. Mnamo tarehe 15 mwezi Julai, mwaka 2002, Sheikh na washukiwa wengine watatu walipatikana na hatia nchini Pakistani, na Sheikh akahukumiwa kifo.
Mnamo mwezi Januari, mwaka 2021, Mahakama Kuu ya Pakistani iliwaachilia waliohusika na utekaji nyara na mauaji ya Pearl. Marekani inatambua vitendo vya wakati uliopita vya Pakistani kumwajibisha Sheikh na inabainisha kuwa Sheikh angali anazuiliwa chini ya sheria ya Pakistani. Serikali ya Pakistani inatarajiwa kuangalia upya chaguzi zake za kisheria ili kuhakikisha haki imetendeka. Marekani pia iko tayari kumshtaki Sheikh kwa makosa yake mabaya mno ya jinai dhidi ya raia wa Marekani.

