Umoja wa Ukombozi wa Kitaifa wa Moro (MNLF)

Asia Mashariki na Pasifiki

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Umoja wa Ukombozi wa Kitaifa wa Moro (MNLF) ulianzishwa nchini Filipino mnamo mwaka 1972. Ulianza kama kundi lililogawanyika kutoka lile la Vuguvugu la Uhuru wa Waislamu. Kundi la MNLF ndilo lililoongoza kwa muda wa karibu miongo miwili kuanzia miaka ya sabini miongoni mwa mashirika ya Moro yaliyotaka kujitenga. Mapema miaka ya tisini, wanachama kadha wa MNLF walijitenga kuanzisha Kundi la Abu Sayyaf (ASG), mojawapo ya makundi ya kigaidi yenye matumizi ya nguvu zaidi nchini Filipino.

Mnamo mwaka 1996, MNLF ilitia saini mkataba muhimu wa amani na serikali ya Ufilipino, na hivyo kuunda Eneo Maalumu la Amani na Maendeleo (SZOPAD). Mwenyekiti wa MNLF Nur Misuari aliteuliwa gavana wa Eneo Huru la Waislamu la Mindanao (ARMM), na ambalo limeundwa na mikoa miwili ya bara na mitatu ya visiwani ambako watu wake, idadi kubwa ambao ni Waislamu, walipewa kiasi fulani cha uhuru wa kujitawala. Mapigano ya mara kwa mara kati ya waasi wenye itikadi kali na vikosi vya usalama vya serikali yaliendelea kwenye eneo la Mindanao, na wengi wa wakazi wa eneo hilo wakatoa wito wa kuanzishwa mfumo madhubuti wa uhuru na maendeleo ya maana katika eneo la Waislamu la Mindanao.

Mnamo tarehe 29 mwezi Septemba, mwaka 2009 kwenye Kisiwa cha Jolo, Filipino, kilipuzi kilichotegwa na MNLF kiliulipua msafara wa magari ya kijeshi. Mlipuko huo uliwaua wanajeshi wawili wa Jeshi la Nchi Kavu la Marekani na mwanajeshi wa Majeshi ya Filipino, ambao walikuwa sehemu ya ujumbe wa wahisani wa kujenga shule eneo hilo.

Mnamo mwaka 2013, watundu wa MNLF walifanya shambulio la matumizi ya nguvu kuzingira kwa wiki tatu Mji wa Zamboanga ambalo liliwaua makumi ya wanachama wa Vikosi vya Usalama vya Filipino na kusababisha maelfu kuhama makazi yao.

Leo, MNLF ina vikundi vingi, baadhi vilivyounga mkono mazungumzo kati ya serikali ya Filipino na kundi lililojitenga la Umoja wa Ukombozi wa Eneo la Waislamu la Moro (MILF). Mazungumzo hayo yalisababisha mnamo mwaka 2018 kupitishwa kwa Sheria Hai ya Bangsamoro (BOL) na kubuniwa mnamo mwaka 2019 kwa Eneo Huru la Bangsamoro la Waislamu la Mindanao (BARMM).

Skip to content