Shambulio la Bomu Dhidi ya Msafara wa Kidiplomasia wa Marekani

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu shambulio la bomu la mwaka 2003 dhidi ya msafara wa kidiplomasia wa Marekani kwenye eneo la Beit Hanoun ndani ya Ukanda wa Gaza. Mnamo tarehe 15 mwezi Oktoba, mwaka 2003, gari lililowabeba maafisa wanne wa usalama wa Marekani lilishambuliwa kwa kilipukaji cha kujitengenezea kilichobebwa na gari, ambacho kiliwaua watu watatu kati yao na kumjeruhi vibaya wa nne. Wahanga hao walikuwa wakiwapa ulinzi wawakilishi kutoka ofisi ya Mjumbe wa Marekani wa Mashariki ya Kati waliokuwa njiani kuelekea Gaza kuwahoji wanafunzi wa Kipalestina walioomba ufadhili wa kiusomi wa Fulbright.

Skip to content