Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu shambulio la bomu la mwaka 1983 dhidi ya kambi ya Jeshi la Marekani la Marine Corps mjini Beirut, Lebanoni. Mnamo tarehe 23 mwezi Oktoba, mwaka 1983, bomu la lori lililipuka katika eneo la makazi ya wanajeshi wa Marekani na Ufaransa waliokuwa sehemu ya Kikosi cha Kimataifa nchini Lebanoni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beirut. Kikosi hiki cha Kimataifa kilikuwa nchini Lebanoni kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kudumisha amani. Shambulio hilo liliwaua wanajeshi 241 wa Marekani na kuwajeruhi wengine 128. Baadaye siku hiyo, wanajeshi 58 wa Ufaransa waliuliwa katika shambulio kama hilo. Hizballah inaaminika kupanga mashambulio hayo, kwa usaidizi na ufadhili kutoka Irani.

