Shambulio la Bomu Dhidi ya Balozi za Marekani (Kenya na Tanzania)

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu mashambulio ya mabomu ya mwaka 1998 dhidi ya Balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania. Mnamo tarehe 7 mwezi Agosti, mwaka 1998, wanachama wa kundi la kigaidi la al-Qa’ida (AQ) sawia walishambulia kwa mabomu Balozi za Marekani Nairobi na Dar es Salaam. Mashambulio hayo yaliwaua watu 224, yakawajeruhi wengine zaidi ya 4,500, na yakasababisha hasara kubwa kwenye majengo ya balozi hizo na uharibifu wa miundo iliyokuwa karibu.

Jijini Nairobi, magaidi walilipua lori lililobebeshwa vilipukaji karibu na maegesho ya ubalozi huo na kuwaua watu 213 — wakiwamo wafanyakazi 44 wa ubalozi (Wamarekani 12 na raia 32 wa mataifa ya kigeni) — na kuwajeruhi watu wengine 4,500, akiwamo Balozi wa Marekani Prudence Bushnell.

Jijini Dar es Salaam, magaidi walioendesha loriu lililobebeshwa vilipukaji walijaribu kuligonga lango la ubalozi, wakapiga risasi masijala ya ubalozi, na halafu wakalipua vilupukaji vyao. Mlipuko huo uliwaua watu 11 na kuwajeruhi 85.

Watu wafuatao walishtakiwa na kupatikana na hatia kwenye mahakama ya serikali kuu ya Marekani kuhusiana na mashambulio hayo:

  • Mamdouh Mahmud Salim, mwanachama mwanzilishi wa AQ, alikamatwa mnamo mwezi Septemba, mwaka 1998 nchini Ujerumani na kurejeshwa Marekani. Anatumika kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusiana kwake na mashambulio hayo ya mabomu.
  • Mnamo mwezi Oktoba, mwaka 2001, majasusi wa AQ Wadih El-Hage, Khalfan Khamis Mohamed, Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali, na Mohamed Sadeek Odeh walipatikana na hatia kwa mashtaka ya kupanga na kutekeleza mashambulio hayo ya mabomu na wakahukumiwa kufungwa maisha gerezani.
  • Mnamo mwezi Januari, mwaka 2011, jasusi wa AQ Ahmed Khalfan Ghailani alipatikana na hatia na akahukumiwa kifungo cha maisha kwa jukumu lake katika mashambulio hayo ya mabomu.
  • Mnamo mwezi Septemba, mwaka 2014, Adel Abdel Bari, mshirika wa karibu wa kiongozi wa AQ Ayman al-Zawahiri, alikiri shtaka la kula njama ya kuwaua raia wa Marekani na kupokea kifungo cha miaka 25 gerezani. Aliachiliwa huru kutoka gerezani mnamo mwaka 2020.
  • Mnamo mwezi Mei, mwaka 2015, Khaled al-Fawwaz, naibu wa kiongozi wa AQ ambaye sasa ni marehemu Usama bin Laden, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusiana kwake na mashambulio hayo.

Jopo la kusikiliza kesi la mahakama ya serikali kuu liliwafungulia rasmi mashtaka Abdullah Ahmed Abdullah, Anas al-Libi, Mohammed Atef, na Usama bin Ladin kwa majukumu yao katika mashambulio hayo. Wote wakiwa viongozi muhimu wa zamani wa AQ, sasa ni marehemu.

Tuzo kwa Mahakama pia tuzo zawadi kwa taarifa kuhusu kiongozi wa AQ Sayf al-Adl, ambaye alishtakiwa kwa jukumu lake katika milipuko ya Ubalozi.

Skip to content