Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu shambulio la USS Cole. Mnamo tarehe 12 mwezi Oktoba, mwaka 2000, walipuaji bomu wawili wa kujitoa mhanga waligongesha dau dogo lililojaa vilipukaji kwenye USS Cole – meli ya Jeshi la Wanamaji la Marekani yenye makombora ya kuelekezwa dhidi ya mashambulio ya ndege – kwenye bandari ya Aden, nchini Yemeni, wakati ilipotia nanga kikawaida ili kuongezwa mafuta. Mlipuko uliotokea ulifungua shimo kubwa kwenye upande wa meli hiyo, ukawaua mabaharia 17, na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30. Shambulio hilo lilipangwa na wanachama wa al-Qa’ida, wakiwamo majasusi ambao sasa ni marehemu Jamal Ahmed Mohammed Ali al-Badawi na Fahd Mohammed Ahmed al-Quso.
