Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Sami Jasim Muhammad al-Jaburi, ambaye pia anajulikana kama Hajji Hamid na Sami Jasim Muhammad al-’Ajuz. Al-Jaburi ni kiongozi mwandamizi wa Dola la Kiislamu la Iraki na Siria (ISIS) na mwanachama wa kurithia wa shirika lililoitangulia ISIS, al-Qa’ida nchini Iraki. Al-Jaburi amekuwa sehemu muhimu katika kusimamia fedha za shughuli za kigaidi za ISIS.
Akitumika kama kaimu wa ISIS kusini mwa Mosul mnamo mwaka 2014, anaripotiwa kutumika katika wadhifa sawa kama waziri wa fedha wa ISIS, akisimamia shughuli za kuongeza mapato ya kundi hilo kutokana na mauzo haramu ya mafuta, gesi, vifaa vya kale, na madini.
Mnamo tarehe 29 mwezi Septemba, mwaka 2015, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja al-Jaburi kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yaa kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya al-Jaburi katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na al-Jaburi. Aidha, ni kosa la jinai kutoa makusudi, au kujaribu kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa ISIS, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.
