Salim Jamil Ayyash

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi kwa taarifa kumhusu Salim Jamil Ayyash, anayejulikana pia kama Salim Jalil Ayyash na kama Jabber. Ayyash ni jasusi mwandamizi wa Kitengo cha 121 cha Hizballah, kikosi cha kutekeleza mauaji cha kundi hilo la kigaidi, ambacho hupata maagizo moja kwa moja kutoka kwa katibu mkuu wa Hizballah Hasan Nasrallah. Ayyash anajulikana kuwa amewahi kuhusika katika juhudi za kuwadhuru wanajeshi wa Marekani.

Mnamo tarehe 11 mwezi Disemba, mwaka 2020, jopo la kimataifa lilimhukumu Ayyash, bila yake kuwepo mahakamani, vifungo vitano vya maisha sambamba kwa mashtaka yanayohusiana na ugaidi kutokana na shambulio la bomu la kujitoa mhanga kutumia lori mnamo mwezi Februari, mwaka 2005 mjini Beiruti ambalo lilimuua aliyekuwa Waziri Mkuu wa Lebanoni Rafik Hariri. Shambulio hilo pia liliwaua watu wengine 21 na kuwajeruhi watu 226. Jopo hilo lilipata kwamba Ayyash aliongoza kundi la mauaji lililomshambulia Hariri, na kwamba Ayyash alishiriki kwenye mauaji hayo siku ya shambulio.

Skip to content