Pambano la Kimapinduzi (RS)

Ulaya na Eurasia

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Kundi la Pambano la Kimapinduzi (RS) liliibuka mnamo mwaka 2003 kutokana na kukamatwa kwa wanachama wa makundi mengine mawili ya Kimaksi ya Uturuki, 17 Novemba na Mapambano ya Watu ya Kimapinduzi. Kundi la kimapinduzi lenye itikadi kali za Kimaksi, RS imefanya mashambulio dhidi ya shabaha za Ugiriki na Marekani nchini Ugiriki. RS kwanza ilipata sifa mbaya lilipodai kuhusika na mashambulio ya bomu ya mnamo tarehe 5, mwezi Septemba, mwaka 2003 dhidi ya Jengo la Mahakama ya Athens wakati wa kusikilizwa kwa kesi za wanachama wa kundi la 17 Novemba. RS ilidai kuhusika na shambulio la makombora ya kurushwa kwa roketi mnamo mwezi Januari, mwaka 2007 dhidi ya Ubalozi wa Marekani jijini Athens na lile la bomu kwenye tawi la Citibank mjini Athens mwezi Machi, mwaka 2009.

Mnamo tarehe 18 mwezi Mei, mwaka 2009, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja RS kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Baadaye, mnamo tarehe 17 mwezi Septemba, mwaka 2009 Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilitaja RS kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya RS katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na RS. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa RS.

Skip to content