Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Murat Karayilan, anayejulikana pia kama Cemal. Karayilan ni kongozi mwandamizi katika Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi (PKK) na ndiye mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Watu ya PKK, kitengo cha kijeshi cha kundi hilo. PKK ni kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.
Mnamo tarehe 14 mwezi Oktoba, mwaka 2009, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Karayilan kama Mlanguzi Mkuu wa Kigeni wa Dawa za Kulevya kuambatana na Sheria ya Kutaja Vigogo wa Kigeni wa Dawa za Kulevya (Sheria ya Kigogo). Matokeo ya kutajwa huku ni kwamba mali yote aliyonayo Karayilan iliyo chini ya mamlaka ya Marekani imezuiliwa, na watu wa Marekani wamekatazwa kufanya miamala yoyote ya kifedha au kibiashara na Karayilan.
