Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu mauaji ya raia wa Marekani Joel Shrum. Mnamo tarehe 18 mwezi Machi, mwaka 2012, Shrum, akiwa na umri wa miaka 29, alipigwa risasi na kuuliwa akiwa njiani kuelekea kazini kwenye eneo la Taizz, nchini Yemeni na mtu mwenye bunduki aliyekuwa akisafiria nyuma ya pikipiki ambayo ilikuwa imesimama kando ya gari lake. Siku chache baada ya shambulio hilo, shirika la kigaidi la al-Qa’ida Kwenye Rasi ya Kiarabu (AQAP) lilidai kuhusika na mauaji hayo.
Wakati wa kifo chake, Shrum alifanya kazi kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo na Maendeleo kama msimamizi na mwalimu wa Kiingereza. Alikuwa akiishi Yemeni na mkewe na watoto wao wawili wadogo.
