Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu mashambulio yaliyofanywa Gaza, Ukingo wa Magharibi, na Israeli ili kuvuruga mashauriano yaliyohusiana na Makubaliano ya Oslo. Tangu kutiwa saini kwa Makubaliano ya Oslo mnamo mwezi Septemba, mwaka 1993, makundi ya kigaidi na watu waliopinga maafikiano ya amani yaliyojadiliwa wamefanya mashambulio kwenye eneo hilo ili kuvuruga mashauriano na kuwashinikiza wadau waliohusika kwenye majadiliano.

