Mashambulio ya Mumbai ya mwaka 2008

Asia Kusini na Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu mashambulio ya mwaka 2008 mjini Mumbai. Kuanzia tarehe 26 mwezi Novemba, mwaka 2008, na kuendelea hadi tarehe 29 mwezi Novemba, mwaka 2008, watu 10 waliopewa mafunzo na Lashkar-e Tayyiba (LeT), iliotajwa na Marekani kama Kundi la Kigaidi la Kigeni, walifanya mfululizo wa mashambulio ya kigaidi yaliyoratibiwa dhidi ya shabaha nyingi mjini Mumbai, India, na kuwaua watu 166. Wamarekani sita waliuliwa wakati wa uvamizi huo ulioendelea kwa siku tatu: Ben Zion Chroman, Gavriel Holtzberg, Sandeep Jeswani, Alan Scherr, Naomi Scherr, na Aryeh Leibish Teitelbaum. Washiriki wakuu kwa njama hii mbaya wangali huru, na uchunguzi bado unaendelea.

David Coleman Headley na Tahawwur Rana walishtakiwa rasmi katika mahakama ya shirikisho ya Marekani kwa kuunga mkono shughuli za kigaidi za LeT. Mnamo mwezi Machi, mwaka 2010, Headley, raia wa Marekani, alikiri makosa kwa mashtaka 12 yaliyomkabili baada ya kukamatwa mnamo mwezi Oktoba, mwaka 2009. Mnamo mwezi Januari, mwaka 2013, Headley alihukumiwa kifungo cha miaka 35 gerezani kwa uhalifu wa jinai ya kigaidi wa shirikisho kuhusiana na jukumu lake katika kupanga mashambulio hayo ya Mumbai na shambulio jingine lililopendekezwa kufuata baadaye dhidi ya gazeti fulani nchini Denmaki. Rana, raia wa Kanada na rafiki wa muda mrefu wa Headley, alihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani kwa kula njama ya kutoa msaada wa nyenzo kwa njama hizo za Denmaki na kulipa msaada wa nyenzo kundi la LeT.

Washukiwa wafuatao pia wameshtakiwa rasmi katika mahakama ya shirikisho ya Marekani:

  • Sajid Mir, meneja wa mradi wa mashambulio ya mwezi Novemba, mwaka 2008, alielekeza mipango, maandalizi, na utekelezaji wa hayo mashambulio;
  • Meja Iqbal, mkazi wa Pakistani, ambaye alishiriki katika kupanga na kufadhili mashambulio yaliyofanywa na LeT;
  • Abu Qahafa, mkazi wa Pakistani na mshirika wa LeT, aliyewapa wengine mafunzo ya mbinu za kivita zinazotumika kwenye mashambulio ya kigaidi; na
  • Mazhar Iqbal, anayejulikana pia kama Abu al-Qama, mkazi wa Pakistani na kamanda wa LeT.
Skip to content