Mahad Karate

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara

Tuzo

Up to $10 million

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni 10 kwa taarifa kumhusu Mahad Karate, anayejulikana pia kama Abdirahman Mohamed Warsame. Karate hutumika kama naibu kiongozi kivuli wa al-Shabaab. Karate ana majukumu kiasi ya ukamanda juu ya Amniyat, kitengo cha al-Shabaab cha ujasusi na usalama, na vilevile juu ya fedha za kundi hilo.

Amniyat ana jukumu muhimu katika kutekeleza mashambulio ya kujitoa mhanga na mauaji ya watu mashuhuri nchini Somalia, Kenya na mataifa mengine eneo hilo, na hutoa usaidizi katika ugavi na usafirishaji wa vifaa kwa shughuli za kigaidi za al-Shabaab. Amniyat ndiyo ilihusika na shambulio la mwezi Aprili, mwaka 2015 dhidi ya Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya ambalo liliwaua watu karibu 150, wengi wao wanafunzi.

Mnamo tarehe 10 mwezi Aprili, mwaka 2015, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Karate kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Karate katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Karate. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa al-Shabaab, iliyotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni.

Skip to content