Kundi la Abu Sayyaf (ASG)

Asia Mashariki na Pasifiki

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Kundi la Abu Sayyaf (ASG) lilijitenga kutoka lile la Moro national Liberation Front mapema miaka ya tisini na ni mojawapo wa makundi ya kigadi yanayotumia nguvu zaidi nchini Phillipines. Likiwa limeshawishiwa na al-Qa’ida mwanzoni, ASG huasisi kuwepo taifa huru la Kiislamu ndani ya eneo la magharibi mwa Mindanao na visiwa vya Sulu. Hivi karibuni zaidi, wanachama wa kundi hilo wameanzisha uhusiano na mshirika wa kieneo wa ISIS, ISIS-Ufilipino. Kundi hilo limetekeleza vitendo vya kigaidi kote Ufilipino, yakiwamo mashambulizi ya bomu, mauaji na utekaji nyara kwa ajili ya malipo.

Mnamo tarehe 8, mwezi Oktoba, mwaka 1997, Wizara ya Mambo ya Nje ilitaja ASG kama Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya Sheria 219 ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Baadaye, mnamo tarehe 23, mwezi Septemba, mwaka 2001, ASG iliorodheshwa katika kiambatanisho cha Amri ya Rais 13224. Kutokana na kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, mali yote na maslahi ya ASG katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na ASG. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa ASG.

Skip to content