Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Junzō Okudaira kwa shambulio la bomu la tarehe 14 mwezi Aprili, mwaka 1988 dhidi ya Klabu ya USO mjini Naples, Italia. Mlipuko huo uliwaua watu watano, akiwamo mwanajeshi wa kike wa Marekani, na ukawajeruhi wengine 15, wakiwamo wanajeshi wanne wa Marekani. Okudaira, mwanachama wa kundi la kigaidi la Jeshi Jekundu la Japani, alifunguliwa rasmi mashtaka nchini Marekani mnamo tarehe 9 mwezi Aprili, mwaka 1993 kwa shambulio hilo kwenye Klabu ya USO. Yeye pia ni mshukiwa katika shambulio la bomu la gari na kombora dhidi ya Ubalozi wa Marekani mjini Roma mnamo mwezi Juni, mwaka 1987.
