Jamal Saeed Abdul Rahim

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Jamal Saeed Abdul Rahim, anayejulikana pia kama Ali Al Jassem Fahd na Ismael. Rahim, anayedaiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Shirika la Abu Nidal, anasakwa kwa kuhusika kwenye utekaji nyara wa tarehe 5, mwezi Septemba, mwaka 1986 wa Ndege ya Pan Am 73 mjini Karachi, Pakistani. Baada ya kuwashika mateka abiria 379 na wahudumu kwa karibu saa 16, watekaji nyara hao walianza kufyatua risasi kiholela. Watu ishirini, wakiwamo Wamarekani wawili, waliuliwa na wengine zaidi ya 100 wakajeruhiwa.

Kwa jukumu lake katika utekaji nyara, Rahim alifunguliwa rasmi mashtaka na jopo kuu la kusikiliza kesi la mahakama ya serikali kuu ya Marekani na yupo kwenye Orodha ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi ya Shirika la FBI. Inaelekea Rahim anaishi Mashariki ya Kati.

Skip to content