Ibrahim Aqil

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 7

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi $7 milioni kwa taarifa kuhusu kiongozi mkuu wa Hizballah, Ibrahim Aqil.

Ibrahim Aqil, ambaye pia anajulikana kama Tahsin, ahahudumu katika baraza kuu zaidi la kijeshi la Hizballah, Baraza la Jihad.

Mnamo muongo wa 1980, Aqil alikuwa mwanachama mkuu wa Shirika la Jihad ya Kiislamu – seli ya kigaidi ya Hizballah – ambalo lilidai kulipua mabomu kwenye Ubalozi wa Marekani mjini Beirut mnamo mwezi Aprili mwaka 1983, shambulio lililoua watu 63, na kwenye kambi ya Wanamaji wa Marekani mnamo mwezi Oktoba, 1983, shambulio ambalo liliua watumishi 241 wa Marekani.

Mnamo muongo wa 1980, Aqil alieIekeza utekwaji nyara wa Wamarekani na Wajerumani Lebanoni na kuwashikilia huko.

Mnamo tarehe 21 mwezi Julai, 2015, Wizara ya Hazina ya Marekani ilimtaja Aqil kuambatana na Amri ya Rais 13582 kwa kuchukua hatua kwa ajili au niaba ya Hizballah. Baadaye, mnamo tarehe 10 Septemba, 2019, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilimtaja Aqil kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa.

Skip to content