Ibrahim Ahmed Mahmoud al-Qosi

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara | Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 4

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni nne kwa taarifa kumhusu Ibrahim Ahmed Mahmoud al-Qosi, anayejulikana pia kama Sheikh Khubayb al-Sudani na Mohammad Salah Ahmad. Al-Qosi ni kiongozi mwandamizi wa al-Qa’ida Kwenye Rasi ya Kiarabu (AQAP), kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.

Al-Qosi alijiunga na AQAP mnamo mwaka 2014, lakini amekuwa mtendaji ndani ya kundi la al-Qa’ida (AQ) kwa muda mrefu na alifanya kazi moja kwa moja kwa marehemu kiongozi wa AQ Usama bin Ladin kwa miaka mingi. Al-Qosi alinaswa nchini Pakistani mnamo mwezi Disemba, mwaka 2001 kabla ya kuhamishiwa Ghuba ya Guantanamo. Alikiri mashtaka mnamo mwaka 2010 mbele ya tume ya kijeshi ya kula njama na AQ na kutoa msaada wa nyenzo kwa ugaidi. Marekani ilimwachilia huru al-Qosi na ikamrejesha nchini Sudani mnamo 2012 kuambatana na makubaliano ya kabla ya kesi.

Tangu 2015, al-Qosi ameonekana katika nyenzo za usajili wa askari na wanachama za AQAP na amehimiza kwenye propaganda za mtandaoni mashambulio ya kutekelezwa na mtu mmoja dhidi ya Marekani. Alitumika kama sehemu timu ya uongozi iliyomsaidia marehemu kiongozi wa zamani wa AQAP shekhe Qasim al-Rimi.

Skip to content