Fuad Mohamed Khalaf

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Fuad Mohamed Khalaf, anayejulikana pia kama Fuad Shongale. Khalaf ni kiongozi wa al-Shabaab na amewezesha usaidizi wa kifedha kwa kundi hili ambalo limetajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni (FTO).

Mnamo mwezi Aprili, mwaka 2008, Khalaf na watu wengine kadha walielekeza mashambulio ya vilipuaji vya kubebwa kwa gari dhidi ya kambi za kijeshi za Ethiopia na maofisa wa Serikali Kuu ya Mpito mjini Mogadishu, Somalia. Mnamo mwezi Mei, mwaka 2008, Khalaf na kundi la wapiganaji walishambulia na kuteka kituo cha polisi mjini Mogadishu, wakawaua na kuwajeruhi wanajeshi kadha. Mwezi huo huo, Khalaf aliandaa hafla mbili za kuichangishia pesa al-Shabaab kwenye misikiti mjini Kismaayo, Somalia.

Mnamo tarehe 13 mwezi Aprili, mwaka 2010, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Khalaf kuwa Raia Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13536 kwa kuchangia matumizi ya nguvuna kuzorota kwa usalama nchini Somalia. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Khalaf katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Khalaf. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa al-Shabaab, kundi lililotajwa kama FTO.

Skip to content