Kuhusu
Chama/Umoja cha Kimapinduzi cha Ukombozi wa Watu (DHKP/C) kilianzishwa mnamo mwaka 1978 nchini Uturuki. DHKP/C hupigania itikadi ya Kimaksi-Kilenini na huipinga Marekani, NATO, na mamlaka ya Uturuki. Kundi hili limelenga maslahi ya Marekani, ikiwa ni pamoja na wanajeshi na wanadiplomasia Wamarekani na majengo yake, wafanyakazi na majengo ya NATO, na shabaha za Kituruki tangu miaka ya tisini. Mnamo mwezi Februari 2013, jasusi wa DHKP/C alilipua bomu la fulana ya kujitoa mhanga kwenye Ubalozi wa Marekani jijini Ankara. Mlipuko huo ulimwua mlinzi wa Kituruki na kumjeruhi vibaya mwanahabari Mturuki. Mnamo mwezi Machi, mwaka 2013, wanachama watatu wa kundi hilo walishambulia Wizara ya Sheria na makao makuu ya chama cha kisiasa cha Kituruki cha Haki na Maendeleo mjini Ankara kwa kutumia makombora na virusha roketi.
Mnamo tarehe 8 mwezi Oktoba, mwaka 1997, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja DHKP/C kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Mnamo mwezi Oktoba, mwaka 2001 Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilitaja DHKP/C kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya DHKP/C katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na DHKP/C. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa DHKP/C.
