Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kwa taarifa kumhusu Ali Sayyid Muhamed Mustafa al-Bakri, anayejulikana pia kama Abd al-Aziz al-Masri. Al-Bakri ni mwanachama wa baraza la shura la al-Qai’da (AQ), chombo cha maamuzi cha kundi hilo, na ni mshirika wa karibu wa kiongozi wa AQ Sayf al-Adl. Al-Bakri ni bingwa wa vilipuzi na silaha za kemikali.
Kabla ya kujiunga na AQ, al-Bakri alikuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Jihad ya Kiislamu la Misri chini ya uelekezi wa al-Zawahiri. Alitumika kama mkufunzi kwenye kambi za AQ nchini Afuganistani, akifunza magaidi kurutu jinsi ya kutumia vilipuzi na silaha za kemikali. Al-Bakri pia alijaribu kuteka nyara ndege ya abiria ya kampuni ya Pakistani Air mnamo Disemba 2000. Inawezekana kwamba anaendelea kuwafunza magaidi wa AQ na watu wengine wenye itikadi kali.
Al-Bakri anaishi na familia yake nchini Irani.
Mnamo tarehe 3 mwezi Oktoba, mwaka 2005, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja al-Bakri kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya al-Bakri katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na al-Bakri. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa AQ, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.
