Al-Mourabitoun

Tuzo

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Kundi la Al-Murabitoun, ambalo mwanzoni lilikuwa sehemu ya al-Qa’ida katika eneo la Kiislamu la Maghreb (AQIM), lilijitenga na kuwa shirika huru mnamo mwishoni mwa mwaka 2012 baada ya kiongozi wake, Mokhtar Belmokhtar, kuachana na AQIM. Baada ya utengano huo, Belmokhtar alitishia kupigana dhidi ya maslahi ya Magharibi na akatangaza kuundwa kwa kikosi cha al-Mulathamun Battalion. Mnamo mwaka 2013, makundi mawili ya al-Mulathamun Battalion na Vuguvugu la Umoja na Jihad Afrika Magharibi (MUJAO) nchini Mali yalitangaza kuwa yangeungana chini ya jina “al-Murabitoun”. Mnamo mwaka 2015, al-Murabitoun ilitangaza kuungana tena na AQIM. Al-Murabitoun iliungana mnamo mwaka 2017 na makundi mengine matatu ya kigaidi ya eneo hilo kuunda Jama’at Nasr al-Islam wal Muslimin (JNIM).

Mnamo mwezi Januari, mwaka 2013, kundi linalojulikana sasa kama al-Murabitun lilidai kuhusika na shambulio dhidi ya kituo cha gesi cha Tiguentourine karibu na In Amenas, kusini mashariki mwa Algeria. Watu zaidi ya 800 walitekwa nyara wakati wa kuzingirwa kwa kituo hicho muda wa siku nne. Raia thelathini na tisa, wakiwamo raia wa Marekani, waliuliwa katika shambulio hilo. Mnamo mwezi Novemba 2015, majajsusi wa al-Murabitoun walishambulia Radisson Blu Hotel mjini Bamako na wakateka nyara watu zaidi ya 170, wakiwamo raia wa Marekani. Watu karibu 27 waliuliwa kwenye shambulio hilo, miongoni mwao mfanyakazi wa Marekani wa maendeleo ya kimataifa. Iliripotiwa kwamba kundi la Al-Murabitoun lilihusika na shambulio lililotekelezwa na AQIM mnamo mwezi Januari, mwaka 2016 kwenye hoteli maarufu ya kitalii nchini Burkina Faso lililoua watu karibu 30, akiwamo raia wa Marekani.

Mnamo mwezi Disemba, tarehe 19, 2013, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja al-Murabitoun, ambayo mwanzoni ilikuwa na jina al-Mulathamun Battalion, kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Awali, mnamo mwezi Disemba, tarehe 18, mwaka 2013, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilitaja al-Mulathamun Battalion kama Kundi la Kigaidi la Kimataifa Lenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Al-Murabitoun linasalia kuwa jina la msingi la kundi hilo. Kutokana na hali hiyo, mali yote ya kundi hilo, pamoja na maslahi yake katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani, vimezuiwa, na watu wa Marekani wanakatazwa kwa jumla kushiriki miamala yoyote na al-Murabitoun/al-Mulathamun Battalion. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa al-Murabitoun/al-Mulathamun Battalion.

Skip to content