Ahlam Ahmad al-Tamimi

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Ahlam Ahmad al-Tamimi, anayejulikana pia kama “Khalti” na “Halati,” kama sehemu ya tuzo yake ya mwaka 1993 ya Matumizi ya Nguvu Dhidi ya Mashauri ya Amani ya Mashariki ya Kati.

Mnamo tarehe 9 mwezi Agosti, mwaka 2001, al-Tamimi alisafirisha bomu na mshambuliaji wa kujitoa mhanga wa Hamas hadi kwenye mkahawa Sbarro pizzeria jijini Jerusalem uliojaa watu, ambapo mshamuliaji huyo alilipua vilipuzi hivyo. Mlipuko huo uliwaua watu 15, wakiwamo watoto saba. Wamarekani Judith Shoshana Greenbaum, mjamzito na mwalimu wa shule mwenye umri wa miaka 31, na mtoto wa umri wa miaka 15 Malka Chana Roth, walikuwa miongoni mwa waliouliwa. Wengine zaidi ya 120 walijeruhiwa, wakiwamo Wamarekani wanne. Hamas ilidai kuhusika na shambulio hilo.

Al-Tamimi, mwanafunzi wa zamani ambaye aifanya kazi kama mwanahabari wa runinga, alimwendesha kwa gari mlipuaji bomu huyo hadi kwenye shabaha hiyo baada ya kuahidi kutekeleza mashambulio kwa niaba ya tawi la kijeshi la Hamas, Izzedine al-Qassam Brigades, kwa mujibu wa FBI. Al-Tamimi, ambaye alipanga na kuliunda shambulio hilo la Sbarro, alichagua sehemu hiyo kwa sababu ilikuwa mkahawa wenye shughuli nyingi. Ili kupunguza tuhuma, yeye na mlipuaji bomu huyo wa kujitoa mhanga walivalia kama Waisraeli, na yeye binafsi alisafirisha bomu hilo, likiwa limefichwa ndani ya mfuko wa gitaa, kutoka mji wa eneo la West Bank hadi Jerusalem. Al-Tamimi pia alikiri kulipua kilipuzi kidogo cha kujitengenezea kwenye duka la vyakula jijini Jerusalem kabla ya shambulio hilo kama jaribio.

Mnamo mwaka 2003, al-Tamimi alikiri mashtaka ya kushiriki shambulio hilo kwenye mahakama ya Israeli na akahukumiwa vifungo 16 vya maisha gerezani nchini Israel kwa kumsaidia mlipuaji bomu huyo. Aliachiliwa huru mnamo mwezi Oktoba, mwaka 2011 kama sehemu ya ubadilishanaji wafungwa kati ya Hamas na Israeli. Mnamo tarehe 14 mwezi Machi, mwaka 2017, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Marekani ilifungua lalamiko la jinai na kibali cha kumkamatwa dhidi ya al-Tamimi. FBI pia ilimwongeza al-Tamimi kwenye Orodha yake ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi.

Skip to content