Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola laki mbili na nusu kwa taarifa kumhusu Ahadon Adak, kamanda katika kundi la Moro National Liberation Front (MNLF).
Mnamo tarehe 29 mwezi Septemba, mwaka 2009, kwenye Kisiwa cha Jolo, nchini Filipino, kilipuzi kilichotegwa na MNLF kiliulipua msafara wa magari ya kijeshi. Mlipuko huo uliwaua wanajeshi wawili wa Jeshi la Nchi Kavu la Marekani na mwanajeshi wa Majeshi ya Ufilipino. Wahanga hao walikuwa kiungo cha ujumbe wa wahisani waliokwenda kujenga shule. Mnamo tarehe 21 mwezi Mei, mwaka 2010, Mkoa wa Tisa wa Mahamaka ya Ufilipino ulitoa kibali cha kumkamatwa kwa Adak kuhusiana na shambulio hilo.
