Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Abdullahi Yare, anayejulikana pia kama Abdullahi Yarisow na Ubeyd. Yare hutekeleza jukumu kuu la kidini ndani ya kundi la al-Shabaab, lililotajwa na Marekani kuwa Shirika la Kigaidi la Kigeni. Hapo awali, Yare aliwahi kuwa mkuu wa vyombo vya habari wa al-Shabaab.
