Abdul Saboor

Asia Kusini na Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kumhusu Abdul Saboor. Saboor ni mtaalamu wa vilipuzi anayehusishwa na Hezb-e Islami Gulbuddin (HIG). Ndiye aliyehusika na shambulio la kujitoa mhanga kwa gari lenye kubeba kilipuzi cha kujiundia (SVBIED) mnamo tarehe 16, mwezi Mei, mwaka 2013 jijini Kabul, Afuganistani. Shambulio hilo liliwaua wanajeshi wawili wa Marekani na wanakandarasi wanne wa Marekani. Mlipuko huo pia uliwaua Waafugani wanane — wakiwamo watoto wawili, ukawajeruhi wengine 37, na kuharibu gari la kivita la Marekani.

Saboor na mtaalamu wa vilipuzi wa HIG Abdullah Nowbahar walikuwa wahusika wakuu kwenye shambulio la SVBIED dhidi ya basi lililokuwa likisafirisha wafanyakazi wa kigeni wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kabul nchini Afuganistani mnamo tarehe 18, mwezi Septemba, mwaka 2012. Mlipuko huo uliwaua watu 12.

Mnamo tarehe 10, mwezi Machi, mwaka 2016, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Saboor kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Saboor katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Saboor.

Skip to content