Abdul Reza Shahla'i

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 15

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi na tano kwa taarifa kuhusu shughuli za kifedha, mitandao, na washirika wa Abdul Reza Shahla’i, anayejulikana pia kama ‘Yusuf Abu al-Karkh’ na Hajji Yusef. Shahla’i ni kamanda wa cheo cha juu katika kikosi cha Irani cha Islamic Revolutionary Guard Corps–Qods Force (IRGC-QF), chenye makao yake mjini Sanaa, nchini Yemen. Shahla’i ana historia ndefu ya kuwalenga Wamarekani na washirika wa Marekani duniani kote.

Shahla’i alipanga mauaji mengi ya wanajeshi wa muungano nchini Iraki, akatoa silaha na vilipuzi kwa makundi yenye itikadi kali ya dhehebu la Shia, na kupanga shambulio la tarehe 20 mwezi Januari, mwaka 2007 Karbala, nchini Iraki, ambalo liliwaua wanajeshi watano wa Marekani na kuwajeruhi wengine watatu.

Kama mfadhili na ofisa wa ngazi ya juu wa IRGC, mnamo mwaka 2011, Shahla’i alifadhili na kuelekeza njama ya kumuua Balozi wa Saudia nchini Marekani jijini Washington, D.C. Shahla’i pia alipanga mashambulio ya kufuatia hilo ndani ya Marekani na kwingineko. Njama zake zingalifaulu, takriban raia 200 wasiokuwa na hatia nchini Marekani wangaliuliwa.

Mnamo tarehe 11 mwezi Oktoba, mwaka 2011, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Shahla’i kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Hapo awali, mnamo mwaka 2008, Wizara ya Fedha ilimtaja Shahla’i kuambatana na Amri ya Rais 13438 kw kutishia amani na utulivu wa Iraki na Serikali ya Iraki. Matokeo ya vitendo hivi, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Shahla’i katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Shahla’i. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo kwa IRGC, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni. Alitajwa pia na Bahareni, Umoja wa Ulaya, Saudia, na Uingereza mnamo mwaka 2018.

Skip to content