Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni ishirini na tano kwa taarifa kuhusu mashambulio ya tarehe 11, mwezi Septemba, mwaka 2001 dhidi ya majengo ya World Trade Center na Pentagon. Magaidi kumi na tisa waliohusishwa na al-Qai’da (AQ) waliteka ndege nne za kibiashara zikielekea California, zikitoka viwanja vitatu tofauti vya ndege mashariki mwa Marekani. Magaidi hao waliangusha ndege mbili kwenye minara mikuu miwili ya majengo ya World Trade Center jijini New York, Jimbo la New York, na ya tatu kwenye upande wa magharibi wa Pentagon, mjini Arlington, Virginia. Ndege ya nne ilianguka karibu na Shanksville, Pennsylvania, huku abiria wakijaribu kuwashinda nguvu watekaji nyara hao. Kwa jumla, mashambulio hayo yaliwaua raia karibu 3,000 wa mataifa ya maeneo yote duniani. Marehemu kiongozi wa AQ, Usama bin Ladin, alidai kuhusika na kupanga na kutekeleza mashambulio hayo kwenye ujumbe wa video baada ya matukio hayo.
Ndege mbili za kwanza, ambazo zilitoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Logan mjini Boston zilitekwa na kuangushwa kwenye minara mikuu ya majengo ya World Trade Center jijini New York. Mgongano wa ndege hizo na moto uliozuka kutokana na mafuta ya ndege yaliyokuwa yakichomeka iliharibu miundo ya minara hiyo hadi ikaporomoka. Shambulio dhidi ya minara hiyo liliwaua watu zaidi ya 2,600.
Ndege ya nne iliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Newark na yamkini ilikusudiwa kwenda kwenye jengo la Bunge la Marekani au Ikulu ya White House. Hata hivyo, abiria waliokuwamo walipigana na magaidi hao ili kuidhibiti ndege hiyo. Kwa sababu ya raia hao jasiri, magaidi hao hawakufikia lengo lao, na ndege hiyo ilianguka karibu na Shanksville, Pennsylvania, ikawaua watu wote 40 waliokuwamo ndani yake.
Ndege ya nne iliondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Newark na inawezekana ilikuwa ikielekea jengo la Capitol au White House Marekani. Hata hivyo, abiria walikabiliana na magaidi ili kuchukua usukani wa ndege. Kutokana na ujasiri wa raia hawa, magaidi hawakufanikiwa kutekeleza shambulizi, na ndege ikaanguka karibu na eneo la Shanksville, Pennsylvania, na abiria wote 40 wakafariki.
Mashambulio hayo ndiyo yaliyokuwa uvamizi wenye maafa makubwa zaidi kutekelezwa dhidi ya Marekani na kundi la nje tangu shambulio la Pearl Harbor mnamo mwaka 1941.
