Mauaji ya Shakeel Khan (Johnson City, New York | 30 Machi, 2019)

Amerika Kaskazini na Kusini | Asia Kusini na Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi $5 milioni kwa taarifa zitakazopelekea kukamatwa au kutiwa hatiani katika nchi yoyote kwa yeyote aliyetekeleza, kujaribu au kula njama kutekeleza, au kusaidia kutenda jinai ya mauaji ya Shakeel Khan.

Mnamo jioni ya tarehe 30 Machi, 2019, Khan, mmiliki-msimamizi wa mgahawa na mkazi halali wa kudumu wa Marekani, aliuliwa kikondoo nje ya mgahawa aliomiliki mji wa Johnson City, New York. Khan alipigwa risasi na mtu mmoja mwenye bunduki wakati akifunga biashara yake usiku huo.

Khan, mwenye umri wa miaka 50 na mzaliwa wa mkoa wa Swat, Pakistan, alihusika wazi katika harakati za kisiasa kupinga mashirika ya kigaidi nchini humo.

Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani katika Wilaya ya Kaskazini ya New York na Kikosi Maalum cha Ugaidi cha FBI wanachunguza mauaji yake.

Skip to content