Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni kumi kwa taarifa zitakazosaidia kuvurugwa kwa taratibu za kifedha za Hizballah. Muhammad Qasim al-Bazzal, anayejulikana pia kama Mohamad Bazzal na Mu’In, ni ofisa muhimu wa Hizballah ambaye majukumu yake ni pamoja na kuleta uwiano wa uhasibu wa kifedha kati ya Hizballah na Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu-Kikosi cha Qods (IRGC-QF).
Al-Bazzal ni mwanzilishi-mwenza wa kampuni laghai inayoonekana kama inafanya biashara halali ya Kundi laTalaqi, yenye makao yake nchini Siria, na anasimamia biashara nyingine zinazofadhili ugaidi, kama vile kampuni ya Hokoul S.A.L. Offshore na Nagham Al Hayat. Kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Kundi la Talaqi, al-Bazzal anasimamia fedha, taratibu, utawala, na mikataba vyote vya kampuni hiyo. Tangu mwishoni mwa 2018, al-Bazzal ametumia kampuni ya Kundi la Talaqi na kampuni zake nyingine kufadhili, kuratibu, na kuficha usafirishaji haramu wa mafuta unaohusiana na IRGC-QF. Al-Bazzal pia amesimamia ubia wa kampuni ya Kundi la Talaqi na ALUMIX, yenye makao yake nchini Lebanoni, kwa ajili ya usafirishaji wa vyuma vya alumini hadi nchini Irani.
Mnamo tarehe 20 mwezi Novemba, mwaka 2018, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja al-Bazzal kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya al-Bazzal katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na al-Bazzal. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa Hizballah, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni. Mnamo tarehe 4 mwezi Septemba, mwaka 2019, Wizara ya Fedha pia ilizitaja kampuni za Hokoul S.A.L., Kundi la Talaqi, Nagham Al Hayat, na ALUMIX kwa kumilikiwa au kudhibitiwa na al-Bazzal.
