Ousmane Illiassou Djibo

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara

Tuzo

Up to $5 million

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Ousmane Illiassou Djibo, anayejulikana pia kama Petit Chapori na Khaled Foulani, kwa kushiriki kwake katika shambulio la mwaka 2017 la Tongo Tongo, nchini Nijeri.

Djibo ni kiongozi wa Dola la Kiislamu la Iraki na Siria Kwenye Sahara Kuu (ISIS-GS) akiendesha shughuli zake kwenye eneo la Menaka nchini Mali. Djibo alikuwa mshirika wa karibu na msaidizi muhimu wa kiongozi wa ISIS-GS ambaye sasa ni marehemu, Adnan Abu Walid al-Sahrawi (Abu Walid). Djibo aliwaelekeza wanachama wa ISIS-GS kuanzisha mtandao wa kuwateka nyara au kuwashambulia raia wa nchi za Ulaya Magharibi nchini Nijeri na mataifa ya karibu. Djibo pia ameshiriki katika mashambulio mengi dhidi ya vikosi vya ndani. Aliwaongoza wapiganaji wa ISIS-GS katika shambulio la tarehe mosi, mwezi Julai, mwaka 2019 dhidi ya kambi ya Majeshi ya Nijeri kwenye kijiji cha Inates, Mkoa wa Tillaberi, Nijeri. Pia aliwaamuru wapiganaji wa ISIS-GS kuwateka nyara wanajeshi sita wa Nijeri wakati wa shambulio la kuvizia dhidi ya wanajeshi wa Nijeri karibu na Tongo Tongo mnamo tarehe 14 mwezi Mei, mwaka, 2019.

Mnamo tarehe 4, mwezi Oktoba, mwaka 2017, karibu na kijiji cha Tongo Tongo, nchini Nijeri, wapiganaji wenye uhusiano na ISIS-GS waliwashambulia wanachama wa Vikosi Maalumu vya Marekani waliopewa jukumu la kufunza, kushauri, na kuwasaidia wanajeshi wa Nijeri kupambana na ugaidi. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani na wanne wa Nijeri. Wamarekani wawili zaidi na Wanijeri wanane walijeruhiwa katika tukio hilo. Mnamo tarehe 12 mwezi Januari, mwaka, 2018, kiongozi wa ISIS-GS wakati huo, Adnan Abu Walid al-Sahrawi, alidai kuhuska na shambulio hilo.

Mnamo tarehe 28 mwezi Juni, mwaka 2021, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilimtaja Djibo kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Djibo katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Djibo. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa ISIS-GS, kundi lililotajwa na Marekani kama Shirika la Kigaidi la Kigeni.

Skip to content