Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni moja kwa taarifa kumhusu Radullan Sahiron, anayejulikana pia kama Kamanda Putol. Tangu mwaka 2005, Sahiron amekuwa kiongozi mkuu wa Kundi la Abu Sayyaf (ASG), lililo na makao yake nchini Filipino, na ambalo limetajwa na Marekani kama Shirika la Kigeni la Kigaidi (FTO).
Sahiron ametenda vitendo kadha vya kigaidi vilivyohusisha mashambulio ya mabomu dhidi ya raia na utekaji nyara wa Wamarekani na raia wa mataifa ya kigeni.
– Sahiron aliamrisha mashambulio ya mabomu dhidi ya Kisiwa cha Jolo mnamo mwaka 2004 ambapo raia 11 wa Filipino na mwanajeshi wa Marekani waliuliwa na wengine zaidi ya 200 wakajeruhiwa. Vilipukaji vya kujitengenezea vilivyotumika katika mashambulio hayo vilitengenezwa kwenye makao makuu ya Sahiron, Kambi ya Tubig Tuh-Tuh, kwenye Kisiwa cha Jolo, Filipino. – Sahiron alihusika kwenye utekaji nyara wa mnamo mwezi Mei, mwaka 2001 ya Dos Palmas wa Wamarekani watatu na Wafilipino 17 kutoka eneo la mapumziko ya kitalii Palawan, nchini Filipinio. Mateka kadha, akiwamo raia wa Marekani Guillermo Sobero, waliuliwa. – Sahiron alichukuliwa kuwa kiongozi muhimu wa utekaji nyara wa mnamo mwezi Aprili, mwaka 2000 kutoka hoteli ya Sipadani, Malesia. Sahiron na wanachama wengine wanne wa ASG waliwateka nyara watalii wa kigeni 21 na wafanyakazi wa eneo la mapumziko ya kitalii, wakiwamo raia wa mataifa ya Ulaya Magharibi, Wamalesia, na Wafilipino.
Sahiron ameshikilia nafasi mbalimbali za ngazi ya juu katika ASG. Mapema sana kama vile mwaka 1999, alikuwa mmoja wa wanachama 14 wa Majlis Shura (baraza la ushauri) ya ASG. Katikati ya mwaka 2002, alikuwa mshauri wa kiongozi wa ASG Khadaffy Janjalani. Hali kadhalika, Sahiron ameshikilia nafasi kadha za uongozi juu ya wapiganaji wa ASG kwenye eneo la Visiwa vya Sulu lililo kusini mwa Filipino. Kutoka mwaka 2000 hadi mwaka 2003, Sahiron alishikilia nyadhifa mbalimbali za uongozi wa ASG, ikiwamo kiongozi wa kikundi cha ASG cha Putol, chenye wanachama wapatao 100 wanaoendesha shughuli zao kwenye Kisiwa cha Jolo kwenye eneo la Sulu lililo kusini mwa Filipinio; kama kiongozi wa kundi la ASG lenye makao yake Sulu likijumuisha makundi 18 yenye silaha; kama Mtadhimu Mkuu wa ASG Sulu; na kama kamanda mkuu wa ASG kwenye Kisiwa cha Jolo akiwa na wafuasi wapatao 1,000 wenye silaha kikamilifu.
Sahiron huenda anajificha kusini mwa Mindanao au Patikul Jolo, Sulu, Filipino.
Mnamo tarehe 27 mwezi Februari, mwaka 2007, Sahiron walifunguliwa rasmi mashtaka kwenye mahakama ya serikali kuu ya Marekani na akashtakiwa kwa kushika mateka. Mamlaka nchini Marekani zilitoa hati ya kukamatwa kwake siku hiyo hiyo. Sahiron yupo kwenye Orodha ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi ya Shirika la FBI.
Mnamo tarehe 28, mwezi Juni, mwaka 2021, Wizara ya Fedha ya Marekani ilimtaja Sahiron kama Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224. Matokeo ya kutajwa huku, miongoni mwa matokeo mengine, ni kwamba mali yote na maslahi ya Sahiron katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na Sahiron. Aidha, ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa FTO ASG.
