Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tatu kwa taarifa kuhusu utekaji nyara wa Kevin Scott Sutay. Mnamo mwezi Juni, mwaka 2013, Vikosi vya Kimapinduzi vya Kolombia (FARC) walimteka nyara Sutay, mwanajeshi wa zamani wa Marekani, karibu na mji wa manispaa ya El Retorno, Kolombia. Sutay alikuwa safarini ndefu kama mtalii kupitia mataifa kadha ya Marekani ya Kati na Kusini.
Mnamo tarehe 9 mwezi Julai, mwaka 2013, FARC ilitoa taarifa ikidai kuhusika na utekaji nyara huo na ikatangaza nia yake ya kumwachilia huru Sutay kama ishara ya nia njema. Hata hivyo, Sutay hakuachiliwa hadi tarehe 27 mwezi Oktoba, mwaka 2013, alipokabidhiwa kwa ujumbe wa serikali za Kolombia, Kuba, na Norwe, na wanachama wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu. Sutay aliachiliwa kwa maofisa wa serikali ya Marekani mjini Bogota, Kolombia, na akarejeshwa Marekani kwa ndege.
