Utekaji Nyara na Mauaji ya William Buckley

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu utekaji nyara na mauaji ya William Buckley. Buckley alikuwa mkuu wa kituo cha CIA nchini Lebanoni, jukumu alilojitolea kuchukua baada ya shambulio la bomu la mwaka 1983 dhidi ya Ubalozi wa Marekani mjini Beiruti ambalo liliwaua watu 63 people, wakiwamo Wamarekani 17. Mnamo tarehe 16 mwezi Machi, mwaka 1984, Buckley alitekwa nyara mjini Beiruti akielekea kazini. Alihojiwa na kuteswa kabla ya kufa akishikiliwa mateka mnamo tarehe 3, mwezi Juni, mwaka 1985. Buckley alikuwa miongoni mwa wahanga 100, wengi wao kutoka mataifa ya Magharibi, ambao Hizballah na magaidi waliohusishwa na Hizballah waliteka nyara na kushikilia mateka wakati wa mgogoro wa mateka Lebanoni ulioendelea kwa muongo mmoja.

Skip to content