Kuhusu
Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu utekaji nyara na mauaji ya mwanajeshi wa Kikosi cha Majini cha Marekani Kanali William Higgins. Higgins alikuwa mmoja wa washiriki wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanoni alipotekwa nyara mnamo tarehe 17 mwezi Februari, mwaka 1988. Watekaji wake walimtesa na kumhoji Higgins kabla ya kumuua. Higgins alikuwa miongoni mwa wahanga 100, wengi wao kutoka mataifa ya Magharibi, ambao Hizballah na magaidi waliohusishwa na Hizballah waliteka nyara na kushikilia mateka wakati wa mgogoro wa mateka Lebanoni ulioendelea kwa muongo mmoja.
