Utekaji Nyara wa Ndege ya TWA Flight 847

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati | Ulaya na Eurasia

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu utekaji nyara wa mwaka 1985 wa Ndege ya TWA 847. Mnamo tarehe 14 mwezi Juni, mwaka 1985, magaidi waliiteka nyara Ndege ya TWA 847 ikiwa safarini kutoka Athens kwenda Roma. Kwa muda wa siku 17, ndege hiyo ililazimishwa kuvuka Bahari ya Mediterania ikiwa na abiria 153 na wahudumu, kutoka Beirut hadi Algiers na kurudi tena, ikatua Beirut mara tatu. Walipotua mara ya kwanza Beirut, watekaji hao walimchapa vibaya, kisha wakampiga risasi na kumuua mpiga-mbizi Robert Stethem wa Jeshi la Majini la Marekani.

Mnamo tarehe 14 mwezi Novemba, mwaka 1985, jopo kuu la kusikiza kesi la mahakama ya serikali kuu ya Marekani ilimfungulia rasmi mashtaka Ali Atwa, Mohammed Ali Hamadei, na Hasan Izz-al-Din kwa majukumu yao katika utekaji nyara huo. Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu kila mmoja wa watu hawa: Atwa, Hamadei, na Izz-al-Din.

Skip to content