Mauaji ya Union Texas Petroleum

Asia Kusini na Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu mauaji karibu na ofisi za kampuni ya mafuta ya Union Texas Petroleum (UTP). Mnamo tarehe 12 mwezi Novemba, mwaka 1997, wafanyakazi wanne wa UTP walikuwa njiani kwenda kazini mjini Karachi, Pakistani. Gari lao la aina ya ‘station wagon’ lilipokuwa likivuka daraja kuelekea jengo la ofisi za UTP, wanaume wawili waliokuwa na bunduki waliruka kutoka kwa gari jekundu aina ya Honda Civic na wakalifyatulia risasi gari hilo. Wafanyakazi wote wanne wa Marekani, pamoja na dereva wao Mpakistani, waliuliwa kwenye shambulio hilo.

Huenda shambulio hilo lilikuwa kulipa kisasi cha kupatikana na hatia kwenye mahakama ya serikali kuu ya Marekani kwa Mir Aimal Kansi siku mbili tu zilizotangulia. Kansi alihusika na mauaji ya mwaka 1993 ya wafanyakazi wawili wa CIA nje ya makao makuu ya shirika hilo sehemu ya Langley, Jimbo la Virginia.

Skip to content