Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki

Mashariki ya Karibu - Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Tuzo

Hadi dola milioni 5

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kumhusu Wadoud Muhammad Hafiz al-Turki, anayejulikana pia kama Sliman Ali Ahmad el-Turki na Bou Baker Muhammad. Al-Turki, anayedaiwa kuwa mwanachama wa Shirika la kigaidi la Abu Nidal, anasakwa kwa jukumu lake katika utekaji nyara wa mnamo tarehe 5 mwezi Septemba, mwaka 1986 wa Ndege ya Pan Am 73 mjini Karachi, Pakistani. Baada ya kuwashika mateka abiria 379 na wahudumu kwa karibu saa 16, watekaji nyara hao walianza kufyatua risasi kiholela. Watu ishirini, wakiwamo Wamarekani wawili, waliuliwa na wengine zaidi ya 100 wakajeruhiwa.

Kwa jukumu lake katika utekaji nyara huo, al-Turki alifunguliwa rasmi mashtaka na jopo kuu la kusikiza kesi la serikali kuu ya Marekani na yupo kwenye Orodha ya Magaidi Wanaosakwa Zaidi ya Shirika la FBI. Mvutaji sigara kupindukia ambaye amefanya kazi kama mhandisi wa ujenzi, Al-Turki inaelekea anaishi Mashariki ya Kati.

Skip to content